Tambua ni Njia gani iliyo Rahisi kwako Kuandika Kitabu (kati Ya hizi 3) ....
March 24, 2022 at 2:28 pm,
No comments

💥Kila mtu ana Njia yake katika Kuandika kitabu👇
Na kila Njia ni sahihi kwa anayeitumia hata kama wengine hawaitumii.
Hapa chini tumeweka njia 3 tu, wewe utaangalia ni ipi unayotumia kwa sasa au utakayoanza kuitumia kuanzia sasa.👇
.
.
💥NJIA YA KWANZA: Kuandikia moja kwa moja kwenye Laptop/Smartphone yako
....kwa kutumia programu tofauti tofauti kama vile Microsoft office, WPS, NotePad, Google docs, n.k.
👉Ni Njia ambayo imekuwa ikitumiwa na watu wengi wasiotulia Eneo moja wakati wa kuandika vitabu. Kwa mfano, watu wanaosafiri mara kwa mara, huku wakiwa na majukumu mengi.
Kwa hiyo, badala ya kukaa Tu kwenye daladala/basi huku wakisikiliza MUZIKI redioni na kusinzia, wao huendelea Kuandika vitabu kupitia vifaa vyao vya kielektroniki (hasa hasa Smartphone).
.....Ila wanaosafiri kwa Ndege hutumia sana Laptop zao.
.
.
💥NJIA YA PILI: Kuandikia kwenye NoteBook/Diary yako
......kwa kutumia Kalamu yako ya wino, halafu baadaye ndipo unakuja kuhamishia kwenye Laptop/smartphone yako; kwa kuandika tena, au kwa kuzi-Scan kurasa halafu unazibadili kwenda kwenye maandishi (text).
👉Hii ni Njia inayotumiwa na watu wengi sana kwa sababu ya Urahisi wake,
.....na pia humpatia Mwandishi uhuru wa Kuandika bila kuhofia kukosea-kosea. Mwandishi anaweza akafanya chochote kile kama apendavyo yeye (hata wakati ambapo kuna MGAO WA UMEME nchini Tanzania) .
.
.
💥NJIA YA TATU: Kurekodi Sauti,
....halafu baadaye unakuja kuipeleka kwenye maandishi (Transcribing).
👉Ni Njia ambayo imekuwa ikitumiwa na baadhi ya waandishi wa vitabu, kwa mfano Mwalimu Christopher Mwakasege (mwalimu wa Neno la Mungu) ambaye huwa anabadili Mafundisho yake ya SAUTI (audio) kwenda kwenye maandishi na kisha kutoa vitabu.
Ukitaka kuamini hilo, nenda kasome vitabu vyake (kwa mfano vile vitabu vya Ndoto), kisha ukasikilize na Mafundisho yake.
Sio huyo tu, hata @titompesa naye alishawahi kutumia Njia hii, @samwel_kibiriti naye alishawahi kuitumia, pamoja na wengine wengi wa ndani na Nje ya nchi ya Tanzania.
.
.
💥Je wewe (mwandishi wa vitabu) ni Njia gani unayopenda kutumia kati ya hizo njia 3❓
Tuandikie hapa chini maoni yako (kwenye Comment)
#lamaxdesigns #lamaxdesigns