STORY: Jifunze kwa Dr. Tony Lewis aliyekuja Kujuta baadaye kwa sababu ya haraka zake za Kuwahi kutoa Kitabu...!
June 13, 2022 at 11:39 pm,
No comments
💥Dr. Tony Lewis alikuwa Ana hamu kubwa sana ya kuona kitabu chake cha kwanza kikiwa kinasomwa na watu wengi sana.

Mara Tu alipomaliza kukiandika, alikuwa ameshapata Oda nyingi sana za Vitabu.
Wengi walikuwa wanataka kumuuzia kwenye maduka yao ya vitabu.
Kutokana na msukumo mkubwa aliyokuwa anaupata kutoka kwa watu mbalimbali, aliamua kuharakisha mambo yake ili awahi kutoa kitabu chake cha "The Message and the Messanger".

👉Alipoambiwa juu ya kumtafuta Mtu mahiri wa kuhariri kazi yake kabla ya kuitoa, alipuuzia kwa sababu hakutaka kutumia Pesa zake kwa watu wengine.
Akamtumia mmojawapo wa Rafiki zake aliyemwambia, "Nimeipitia kazi yako, ni nzuri sana."
Cha ajabu sana,
Hata yeye mwenyewe hakutaka kuipitia kazi yake kwa sababu aliamini yupo BIZE sana.
Chapu chapu akaenda kukichapa na kuanza kukisambaza.
👉Lakini siku iliyofuata, dada yake alimpigia Simu na kumwambia, "Umekiona vizuri kitabu chako?"
Akamjibu, "Una maanisha nini?"
"Kitabu chako kina Matatizo mengi sana"
Akapiga picha baadhi ya kurasa za kitabu na kumtumia.
Dr. Lewis alijisikia vibaya sana kwa kutokuyaona hayo yote mapema kabla ya kuchapa kitabu chake.
Kilichofuata...
Akaamua kutupilia mbali Vitabu vyake vyote alivyovichapa.
Akajikuta ameingia kwenye Gharama kubwa sana kuliko ya Awali [ya kumlipa mtu mahiri atakayeipitia kazi yake na kuirekebisha].
Sasa, Inawezekana nawe ni kama Dr. Lewis
👉Umekuwa na tabia ya kujiona mkamilifu, huna haja ya kumtafuta na kumlipa Mtu mwingine mwenye Uwezo wa kuihariri kazi yako kwa Uzuri zaidi.
Ukishamaliza kuiandika na kuipitia Mara moja au mbili haraka haraka, unakimbia kwenda kuichapa ili uanze kuingiza pesa na kuitwa Mwandishi wa Vitabu.
Ila usichojua ni kwamba, UNAJIHARIBIA MWENYEWE.
👉Watu wakishaona kitabu chako kina makosa mengi ya ajabu ajabu, basi huishia kukiweka Pembeni bila kukisoma, na kisha kuapa kutokununua tena Vitabu vyako vingine wakiamini navyo vitakuwa na makosa mengi ya kiuandishi.
Sasa......
Habari Njema ni kwamba, @lamaxdesigns tumekuja kukusaidia.
Je, umeandika kitabu cha kiroho, au cha Biashara na Ujasiriamali, au cha Uelimishaji?
Kilete Leo tukihahariri kwa Uzuri zaidi.
💥Mawasiliano: 0764 793 105 WhatsApp.
@lamaxdesigns.
.