Epuka HAYA MAKOSA katika Uandishi wa Kitabu chako (sehemu Ya 5)
April 12, 2022 at 11:56 am,
1 comment
💥SWALI: Je, Mpaka sasa umekwisha kufanya MAKOSA mangapi kwenye safari yako ya Uandishi wa Vitabu ?
Tunaamini sio tu mawili au matatu, ni Mengi sana.
...kuanzia kwenye Alama za uandishi, upangiliaji wa sentensi na aya, matumizi ya mifano na Nukuu, lugha ya Picha, pamoja na mengine mengi.
Na hata Sasa, yamkini umetoka kukosea tena.
Ila, pamoja na hayo yote, @lamaxdesigns tupo hapa kusaidiana nawe ili kwa pamoja tuweze kuwa na Kazi Nzuri zitakazoisaidia Jamii yetu kufanikiwa katika mambo yote, na kisha kustawi.
Katika mfululizo wa hili Somo, tumekwisha kuangalia zaidi ya Makosa matatu. Na Leo tunaendelea na kosa la tano.
[Pitia kwenye Tovuti yetu Upate masomo ya Awali].
Kabla ya kuingia kwa Undani zaidi, tuanzie hapa...
👉Hivi ulishawahi kusoma kitabu ambacho kilikuwa kinakuhitaji kuingia 'Google' kila wakati, au kufungua kamusi (dictionary) kuangalia maana ya maneno fulani fulani?
Je, Ulijisikiaje?
Na
Je, hali hiyo ilikupatia hamasa ya kuendelea kukisoma hicho kitabu kwa Bidii kubwa sana, au ulichoka na kuamua kwenda kuendelea na Shughuli zako nyingine?
Tunachoamini ni kwamba, Hamasa yako ilipungua kwa zaidi ya Asilimia sabini (70%).
Na hata kama ulijitahidi kuendelea nacho, Basi ilikuwa ni kwa sababu ya kukosa kazi nyingine ya kufanya.
Hilo ndilo KOSA Mojawapo kubwa linalofanywa na Waandishi wengi.
...Wengi hutumia MISAMIATI migumu sana karibia kwenye kila Sura ya kitabu. Jambo linalomfanya msomaji kupata wakati mgumu; kwa Sababu kila wakati anakuwa anakiweka kitabu Pembeni ili atafute maana ya misamiati iliyotumiwa.
Kama wewe ni mmojawapo wa Waandishi wa aina hiyo, Basi achana na hiyo tabia kuanzia sasa.
Kwani dhamira yako ya kuandika hicho kitabu ni kumkomoa msomaji wako na kumfanya ajutie uwamuzi wake wa kununua hicho kitabu chako?
Kama sivyo, Basi angalia namna ya kutumia maneno yanayoeleweka kirahisi.
Usiwaingize Wasomaji wako kwenye mtego wa kugharamika zaidi katika kununua tena kamusi na kutembea nazo njiani kama vile Wanafunzi wa Sekondari.
👉Hata kama ni misamiati inayokufurahisha sana, itumie kufurahia nyumbani kwako, siyo kwenye kitabu kinachosomwa na mamia ya Watu wenye viwango tofauti tofauti vya uelewa.
Umeelewa?
Tuachie hapa chini maoni Yako 👇
1 comment - Epuka HAYA MAKOSA katika Uandishi wa Kitabu chako (sehemu Ya 5)
Hekima Mwasile - April 19, 2022 at 11:10 am
Umeandika madini makubwa Kaka, imekaa poa mno, Ngoja nipitie na ya awali