UNATAKA KUJUA KAMA KITABU CHAKO KITAUZIKA SOKONI? (Soma hapa)
April 17, 2022 at 9:26 pm,
No comments
Ni Rahisi sana
Kama kumsukuma Mlevi aliyesimama juu ya Utelezi.
Cha kufanya ni hiki...
Jaribu KUJIUZIA wewe Mwenyewe.
Kivipi?
Vaa kiatu cha MTEJA.
Jifanye wewe ndiye Mteja unayetaka kumuuzia hicho kitabu chako, na wala HUMJUI KABISA Mwandishi wake.
Baada ya hapo...
Ebu Jiulize,
Je, Unaweza ukanunua kitabu chenye TITLE ya namna hiyo ?
Je, Unaweza kushawishika kununua kitabu chenye Muonekano huo ?
Je, Unaweza ukanunua kitabu ambacho Mwandishi wake amejieleza kwa namna hiyo ?
Je, kitabu kinakutamanisha kujua yaliyomo ndani yake ?
UKIGUNDUA
Hata wewe Mwenyewe una mashaka, hapo utakuwa umekwisha kupata Jibu lako kamili.
Hicho kitabu kitakutesa sana Sokoni.
Ikitokea ukauza, basi ni kwa Watu wachache WALIYOAMUA KUKUUNGA MKONO; kama wasemavyo vijana wa kibongo.
Hivyo, huna budi KUBADILI au KUREKEBISHA CHOCHOTE KILE KILICHOKUFANYA USHINDWE KUNUNUA KITABU CHAKO.
Nje ya hapo, "Utavunjika guu."
Umeelewa ?
Ikiwa Unahitaji ushauri wa karibu zaidi, pamoja na huduma zitakazokusaidia kuwa na Matokeo chanya Sokoni, FOLLOW @lamaxdesigns @lamaxdesigns.
WhatsApp 0764793105.
Kumbuka: Kesho Bora Inatengenezwa Leo.
ÂŠī¸ LAMAX DESIGNS.
@lamaxdesigns.
Founder: @lacksontungaraza.
#SHARE