SIRI: Jinsi Hofu ilivyoninyima Kuuza vitabu vingi...
October 3, 2022 at 1:33 pm,
No comments

Sikuwahi kufikiria kama Ujinga unaweza ukamfanya mtu apuuzie mambo ya msingi na baadaye kuanza kujutia Ujinga wake.
Nakumbuka...
💥Mara ya kwanza nilipotoa kitabu, nilikumbana na Changamoto kadhaa.
...Mojawapo ilikuwa ni katika Usambazaji.
Ilikuwa inaniwia ugumu kuwafikishia watu wa mbali mahitaji yao ya vitabu kwa gharama zilezile.
Ilikuwa ni Lazima mtu alipie na gharama za Usafiri ili apate kitabu chake. [Kwa wakati huo nilikuwa mkoani Dodoma].
Sasa, fikiria, kitabu ni shilingi Elfu tano, halafu tena mteja anatakiwa kulipia shilingi Elfu tano nyingine kwa ajili ya Nauli ya kumtumia kitabu kwa Njia ya Basi.
...Jambo ambalo ni sawa na kununua Vitabu viwili.
💥"Naomba utuuzie soft copy basi, maana Sisi wa mbali unatuumiza." Ndivyo nilivyokuwa nikiambiwa na Wateja wa mbali.
Lakini nikaendelea kushupaza Shingo kwa kuwajibu, "Mimi nauza hard copy Tu;" Kama Nawe unavyowaambia sasa hivi.
Kwa jinsi hiyo, Nikawa napitwa na Pesa nyingi sana mbele yangu.
Kilichokuwa kinanitesa sio kingine mbali na Hofu.
💥Kila wakati nilikuwa ninahofia watu kuanza kusambaza Vitabu vyangu BURE kwa wenzao baada ya Mimi kuwatumia Vitabu kwenye EMAIL na WhatsApp; kama nawe pia unavyohofia hata sasa.
Nilipokuja kushituka, sikuweza kuwapata tena wale Wateja wa Awali kwa sababu Sikuwa na Mawasiliano nao na wengine walikuwa wamekwisha kubadili vipaumbele vyao.
🛑Kwanini nimeamua kukuambia hayo yote?
Nataka #Usipitwe na Fursa za maana maishani mwako kwa sababu ya Hofu.
Lakini pia usiwe na Ujasiri uliyopitiliza kabla ya kuchukua tahadhari za Awali.
💥WEWE ULIYE MWANDISHI WA VITABU...👇
"Kubali kuendana na Mahitaji ya Soko zaidi ya mahitaji yako binafsi."
Using'ang'anie kuuza Vitabu vyako vya 'hard copy' Ikiwa Soko linahitaji 'Soft copy'; Hapo utakuwa unapishana na Gari la mshahara.
Utaniuliza, "Vipi sasa kuhusu usalama wa kazi yangu ili watu wasiweze kuisambaza Bure Mtandaoni bila idhini yangu?"
Hilo lisikutie Shaka.
Nimekwisha kupata Mfumo mzuri sana utakaokusaidia kuuza kazi zako kwa usalama mkubwa kwa Wateja wako waliopo popote pale duniani, huku ukiendelea kupata Pato lako unalostahili.
Utaniuliza tena, "Ndiyo Mfumo gani huo na unafanyaje kazi?"
Hilo nalo lisikutie Shaka kabisa.
Njoo Sahivi WhatsApp kwa nambari 0764 79 31 05, nikujuze.
💥Kumbuka: Kujiunga na Kuutumia huo Mfumo ni Bure kabisa. Hivyo usiwaze juu ya Ada ya kujiunga.
[Nafasi zipo 9 Tu kwa Leo. Wahi mapema]
By LACKSON TUNGARAZA.
Mwandishi wa Vitabu na Mkufunzi wa Waandishi wa Vitabu na Wajasiriamali.